MKURUGENZI WA WASHAWASHA CLASSIC MIN BAND AIBUKA NA BENDI MPYA... ni "Halichachi Classic Modern Taarab"

ALIYEKUWA kiongozi mwandamizi wa Washawasha Classic Modern Taarab iliyovunjika hivi karibuni, Amour Maguru hatimaye ameibuka na bendi mpya iitwayo ‘Halichach Classic Modern Taarab’, imefahamika.

Tayari Halichachi Classic imeanza kufanya shoo ambapo inatumbuiza kwenye kumbi na maeneo tofauti za burudani jijini Dar es Salaam pamoja na kwenye mialiko ya sherehe mbalimbali.

Akiongea na saluti5, Amour ambaye ni gwiji la kupapasa kinanda, amesema Halichachi Classic inakusanya baadhi ya wasanii waliokuwa wakiunda bendi ya Washawasha Classic.

“Nawaomba mashabiki kunisapoti kikamilifu ndani ya Halichachi Classic kama ilivyokuwa kwenye bendi iliyosambaratika ya Washawasha, nawaahidi mambo mengi matamu ikiwa ni pamoja na nyimbo zetu wenyewe,” amesema Amour.


Amesema kuwa, japo anasikitika sana kuvunjika kwa Washawasha, lakini hana budi kuyasahau yaliyopita na kuwataka mashabiki kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuyafikia malengo ya kimuziki.

No comments