MOHAMED ALLY “MTOTO PORI” AKWEA JUKWAA LA JAHAZI NA KUSEMA MASHABIKI 'WANAIHARIBU' TAARAB


Mwimbaji wa Wakali Wao Modern Taradance, “Mohamed Ally "Mtoto Pori”, Jumapili iliyopita aliitembelea bendi yake ya zamani Jahazi Modern Taarab na kuimba wimbo wake “Kazi Mnayo” uliotesa kwenye albam ya “Wasi  Wasi Wako…” iyotoka mwaka 2012.

Mtoto Pori akateka hisia za mashabiki wa Jahazi waliofika Traveritine Hotel, Magomeni ambao walitaka aimbe pia wimbo wake wa “Tuacheni Tulivyo”, lakini mwimbaji huyo  akawaahidi kurejea tena ukumbini hapo Jumapili ijayo.

Pamoja na hayo, Mtoto Pori alitumia fursa hiyo kuwaomba mashabiki wa taarabu wasapoti bendi zote na waache kutupiana lugha za matusi kwenye mitandao ya kijamii.

“Wasanii tunapendana sana lakini mashabiki mnaharibu, mnatuingiza vitani hadi baadhi yetu tunashindwa kusalimiana,” alisema Mtoto Pori.

“Punguzeni lugha za matusi kwa wasanii msiowapenda, mnatupa shida sana, hao hao mnaowatukana ndio marafiki zetu tunaoshirikiana kwa hali na mali, mnahatarisha sana mahusiano baina ya wasanii na wasanii, bendi na bendi,” aliongeza mwimbaji huyo aliyejiunga na Wakali Wao mwaka jana.


No comments