MONACO YAITAKA ARSENAL ICHEUE EURO MIL 61 ILI KUMNASA THOMAS LEMAR

KLABU ya AS Monaco imeitangazia dau Arsenal ambayo inamtaka nyota wao, Thomas Lemar, baada ya kusema itakuwa tayari kumwachia endapo itajikamua kitita cha Euro milioni 61.


Gazeti la Daily Star liliripoti juzi kuwa mabingwa hao wa Ufaransa wanasema hawatakuwa na hiyana kumwachia kiungo huyo kwa vinara hao washika bunduki kutoka Kaskazini mwa jiji la London kama watafikia dau hilo.

No comments