MOURINHO AWAMBIA MASHABIKI WAKE "MSIJALI, POGBA BADO ANA NAFASI"

KOCHA wa sasa wa Manchester United, Jose Mourinho amewaambia mashabiki wa klabu hiyo hawana haja ya kuhofia ujio wa wanandinga wapya wanaosajiliwa msimu huu kwa kuhofia alivyomaliza msimu uliopita vibaya kiungo Paul Pogba.

Pogba alisajiliwa na mashetani wekundu wa jiji la Manchester akitokea katika kikosi cha Juventus ya Italia.

Akinukuliwa na tovuti ya klabu ya United, kocha huyo raia wa Ureno alisema: “Ingawa msimu uliopita hakuonesha makeke yake ya kawaida, lakini ninachoamini ana nafasi ya kung’ara zaidi msimu huu”.

Kauli ya Mourinho inakuja siku si nyingi alipotanabaisha azma yake ya kumwandaa Pogba kucheza sambamba na mshambuliaji ‘Kibabu’ Zlatan Ibrahimovic ambaye naye alianza kwa makeke akiwa kikosini, lakini hakumaliza vizuri kasababu ya kuwa majeruhi”.

Awali Mourinho amewahi kunukuliwa akisema, alifanya uamuzi sahihi kumwita kundini Pogba na kwamba hatua yake hiyo itazaa matunda ifikapo mwishoni mwa msimu.

Aliyasema hayo baada ya kuwapo kwa lawama za kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka wa ndani na nje ya England waliouponda usajili wa msimu uliopita huku wakionesha mashaka pia kwa wachezaji wanaosajiliwa msimu huu.


Tayari Mourinho ameshawasajili wachezaji kadhaa wakiwemo Victor Lindelof na Lomelu Lukaku ambao hata hivyo tayari wameanza vyema katika mechi za awaliza kujiandaa na msimu ujao wakiwa nchini Marekani.

No comments