MREMBO NADIA BUARI WA FILAMU GHANA AJIPANGA KUREJEA TENA KWENYE GEMU

 NADIA Buari, staa wa filamu anayetajwa kuwa na mvuto zaidi wa kimapenzi nchini Ghana, amesema kuwa anajiandaa kuendelea na kazi ya uigizaji baada ya mapumziko ya muda mrefu.

Nadia alikuwa nje ya ulingo wa sanaa baada ya kuwa na ujauzito ambapo amejifungua watoto mapacha ambao kabla alikuwa akiwaficha wasionekane kwenye mitandao ya kijamii.

“Ilinilazimu kujiweka kando kwanza kwa sababu nilikuwa kwenye maandalizi ya kuitwa mama, nashukuru kila kitu kimekwenda sawa, nimebahatika kupata watoto wawili,” alisema nadia.

“Sanaa ya uigizaji ni sehemu ya fani yangu, najaribu kuona ni kwa namna gani nitarejea upya nikiwa na mwonekano mwingine kabisa,” aliongeza staa huyo.

Tangu apate ujauzito, amekuwa akiishi maisha ya kuficha akihofia kupigwa picha na wanahabari na kwa mara ya kwanza alirusha picha akiwa sambamba na watoto wake pamoja na mzazi mwenzie.

No comments