MRITHI WA CANNAVARO YANGA ASIKITIKA KUIKOSA JEZI NAMBA 13

Beki mpya wa Yanga SC, Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amekabidhiwa vifaa vya mchezo na wadau wake waliopo kisiwani Zanzibar.

“Nawashukuru sana mashabiki wangu ambao wamekuwa nami toka naanza kucheza soka binafsi, napenda kuvaa jezi namba 13, hiyo jezi nimekuwa nikiipenda tangu zamani sababu kuna shabiki wangu mmoja wakati najiunga na Taifa Jang’ombe aliwahi kuniambia huwa anapenda anione nikiitumia kwa kuwa namkubali nikiaona niitumie na nimekuwa nikiipenda sana."

“Nimekuja Yanga wamenipa jezi namba sita kutokana na ile niliyokuwa naipenda kuwa na mtu, sikuwa na jinsi kwa sababu naamini hata ii haiwezi kuniharibia kitu kwenye malengo yangu ndani ya Yanga ingawa ningepata ninayotaka ingekuwa vizuri,” alisema Ninja.


Wiki iliyopita mashabiki walifika kumpokea Ninja  alipowasili akitokea Tanzania bara, mashabiki hao walianza kumpokea tangu bandarini Malindi na kumpandisha gari aina ya Canter hadi nyumbani kwao Jang’ombe huku njiani wakimwimbia nyimbo na kupiga dufu kuashiria furaha ya mpendwa wao huyo kusajiliwa Yanga.

Ninja anatajwa kama mrithi wa Nadir Haroub Cannavaro.

No comments