MSIKILIZE TX MOSHI WILLIAM ALIVYOTESA KWENYE WIMBO “WIVU SINA” WA POLISI JAZZMNAMO mwaka 1979, Polisi Jazz Band wakati huo ikiwa kwenye chati kabisa, chini ya uongozi wake Shukuru Majaliwa aliyekuwa mpuliza tarumbeta mahiri, ilipakua kibao “Wivu Sina” ambacho hadi leo kinaendelea kuwa kwenye ubora wake.

Saluti5 imeamua leo kukukumbusha wimbo huu ambao umetungwa na marehemu Kassim Mapili aliyeshiriki kucharaza gitaa la solo, huku rithym ikiwa imepigwa na Jimmy Menssah na Bosco Mfundili kwenye bass.


Waimbaji walikuwa ni Moshi William, Primo Gandamo, Jalala Ally na Idrisa Pokwe aliyekuwa pia akikung’uta tumba. Drums utakazozisikia kwenye kibao hiki zimecharazwa na Manzi Mbwana.

No comments