MSUVA: NIKO TAYARI KWENDA KUANZA MAISHA MAPYA YA SOKA LA KULIPWA

MCHEZAJI wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva sasa yuko tayari kwenda kuanza maisha mapya ya soka la kulipwa nje ya Tanzania na hii ikiwa ni mara yake ya kwanza.

“Kila kitu kipo tayari, naondoka wakati wowote kuanzia leo (jana).”

“Nitaelekea Morocco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida ambao ni washindi wa pili Ligi Kuu Morocco. Naondoka Yanga SC, timu uliyonilea na kunipa mafanikio.”

Msuva ameongeza kwa kusema: “siondoko kwa ubaya ndio maana nimefuata taratibu zote ambapo viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara, naamini iko siku nitarudi kuitumikia Yanga tena, ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya na kuwa miongoni mwa wanasoka waliofanikiwa nchini.”

“Bada ya Morocco Mungu akijaalia basi nitakuwa Ureno, lakini hasa ni Hispania maana nina uwezo wa kucheza la Liga.”


Mchezaji huyo amemalizia kwa kuwashukuru wana Yanga kwa ushirikiano mkubwa waliompatia, anaamini kupitia kipaji chake, iko furaha amewapa wapenzi wa klabu hiyo.  

No comments