MTIBWA SUGAR WAAMUA KUWAGEUKIA WACHEZAJI WANAOCHIPUKIA USAJILI WA MSIMU HUU

WAKATI klabu za Ligi Kuu Bara zikitunishiana misuli ya kumwaga fedha katika kipindi hiki cha usajili, wenyeji wa mkoa wa Morogoro timu ya Mtibwa Sugar wao wamegeukia makinda wanaochipukia.

Mtibwa ambao wamekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa JKT Oljoro, Husseni Iddy, mpango wao ni kuinua wachezaji wapya ambao hawajawahi hata kucheza michuano ya Ligi Kuu Bara.


“Tuna vijana wengi wenye uwezo kutoka kikosi cha pili ambao tuna imani wanaweza kutuvusha kuliko kuhangaika na wachezaji ambao umri umeshaenda,” alisema Ofisa Habari wa klabu hiyo, Thobias Kifaru.

No comments