MTOTO WA BOB MARLEY KUMPA KOLABO JAY Z

MTOTO wa marehemu Bob Marley, Damian Marley ameweka wazi kuwa yuko kwenye mipango ya kufanya kazi na rapa Jay Z.

Wiki iliyopita rapa huyo alikuwa nchini Jamaica ambapo alionekana akiwa na Damian, hata hivyo kupitia akaunti ya Instagram, Damian ameweka wazi kuwa anatarajia kufanya wimbo mmoja na rapa huyo wa Marekani.

“Nimetumia muda mwingi kuzungumza juu ya kufanya muziki. Kila kitu kimekwenda sawa na kilichobaki ni kuwafurahisha mashabiki. Nimeweza kutum ia nafasi niliyopata ya kukaa na rapa huyo hivyo sitaki kuchelewesha mashabiki, nataka kuvunja amani kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo mbalimbali vya habari,” aliandika Damian.


Hata hivyo, Jay Z yuko katika maandalizi ya ziara yake ya kimuziki nchini Jamaica, kwa mujibu wa Damian.

No comments