MTOTO WA GEORGE WEAH AJINASIBU KUVAA VIATU VYA BABA YAKE KATIKA SOKA

TANGU Thomas Weah ambaye ni mtoto wa mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Liberia, Gegre Weah atangaze kujiunga na klabu ya PSG, kumekuwa na hisia tofauti.

Baadhi ya mashabiki wanasema hawaoni kama Thomas ana kiwango kivuri kumfikia baba yake lakini yeye mwenyewe amesema kwamba atahakikisha anafuata nyao za baba yake.

“Nitahakikisha kwamba nafuata nyayo za baba yangu, nataka kucheza kwa kiwango kikubwa na watu watashangaa,” amesema Weah huyo mdogo.

Tomothy Weah amesema ameamua kufuata nyayo za babake ambaye ni mshindi wa taji la Ballon d’Or Geogre Weah baada ya kutia saini kandarasi na klabu hiyo ya PSG.

Mshambuliaji huyo mwenye uri wa miaka 17, ametia saini mkataba wa miaka mitatu na PSG klabu ambayo George Weah aliwakilisha kutoka mwa 1992 hadi 1995.

Amesema awali ya hapo kulikuwa na uvumi kabisa kwamba anafuata nyayo za baba yake na hicho ndicho anataka kukifanya.

Mnamo mwezi Septemba 2016 Weah huyo mdogo alifunga “hattrick” katika ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya klabu ya Ludogorets katika mechi yake ya kwanza ya UEFA.

“Ni fahari kubwa kuendeleza pale baba alipoachia,” alisema Weah ambaye alizaliwa mjini New York na kujiunga na New York Red Bulls kabla ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya soka cha PSG mnamo mwezi julai 2014.

“Niko kwenye klabu, kubwa na natumai nitaendelea kuimalika ili kuchezea timu kubwa.”

Baba yake mwenye umri mia 50 kutoka Liberia aliwahi kushinda mara tatu taji la mwanasoka bora wa Afrika na taji la Ballon d’Or mwaka 1995.

Alijipatia umaarufu katika klabu ya Monaco 1988 na kufanikiwa kuichezea PSG na AC Milan muongo uliofuata.

Pia alichezea Chelsea na Man City katika Ligi ya Uingereza katika miaka ya mwisho ya soka yake.

No comments