MWADUI FC KUINGIA KAMBINI MWISHONI MWA WIKI KWA AJILI YA MAANDALIZI YA LIGI

WAKATI timu kadhaa zikiwa zimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania bara, kwa upande wa Mwadui FC wanatarajia kufanya hivyo kati ya mwishoni mwa wiki au wiki ijayo.

Kocha wa kikosi hicho, Ally Bushiri alisema kuwa ndani ya siku chache hizi atawakusanya vijana wake kuingia kambini rasmi.

“Kati ya mwisho wa wiki au wiki ijayo tutakuwa tayari tuko kambini kwa ajili ya kujifua ambapo kama muda ukiwepo wa kutosha tutacheza michezo kadhaa ya kirafiki.”


“Kwa upande wa usajili bado tuko kwenye mazungumzo na wachezaji kama watatu hivi na mambo yakienda sawa watasaini kuitumikia Mwadui kwa msimu ujao,” alisema.

No comments