Habari

MWAKA WA SHETANI!!! SANCHES APEPERUKA MANCHESTER UNITED

on

Manchester United inaelekea kumkosa kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches aliyekuwa akiwindwa na kocha Jose Mourinho.
Kiungo huyo wa Kireno aliyeitosa Manchester United msimu uliopita na kuchagua kutua Bayern Munich, alihusishwa tena na safari ya Old Trafford kiangazi hiki baada ya Bayern kusema kuwa ipo tayari kumpiga bei mchezaji huyo.
Hata hivyo Sanches sasa anaelekea kutua AC Milan baada ya gazeti la L’Equipe la Ufaransa kudai kuwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, anakwenda San Siro kwa dau la pauni milioni 35.
Gazeti hilo limedai Sanches atasaini mkataba wa miaka minne kuitumikia miamba hiyo ya Italia. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *