MWAKA WA TAABU NI WA TAABU!... HIMID MAO NAE KUIKIMBIA AZAM

KLABU ya Azam ambayo imekumbwa na tatizo la kukimbiliwa na mastaa wake wakubwa inaelekea tena kukimbiwa na kiungo wake mkabaji Himid Mao Mkami aliyeweka wazi kuwa akili yake inafikiria namna ya kuondoka hapa nchini.

Mao amesema kuwa amepata ofa nyingi za kucheza nje ya nchi, za Afrika Kusini na Dermark hivyo anafanya mawasiliano ya karibu na wakala wake ili aweze kukamilisha safari hizo.


Azam mpaka hivi sasa imeshakimbiwa na mastaa wake wakubwa ambao walikuwa muhumili wa miaka mingi akiwemo Erasto Nyoni na John Bocco ambao wamedumu kwa muda mrefu kwenye kikosi hicho.

“Kwakeli niwe muwazi tu, hivi sasa akili yangu haipo hapa tena, nawaza kusonga mbele zaidi, nadhani ni wakati sahihi wa kucheza soka nje ya nchi,” alisema Himid.

No comments