STAA wa mipasho mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Mwanahawa Chipolopolo yuko kambini na bendi yake mpya ya Halichachi Classic Modern Taarab akisuka kibao kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Nilijua yatakushinda’.

Taarifa kutoka ndani ya halichachi Classic zinasema kuwa kibao hicho kinaweza kuwa cha kihitoria kwa mwaka huu kutokana na namna kinavyopangiliwa kwa ustadi mkubwa kwenye sauti na ala.

Ndani ya ‘Nilijua Yatakushinda’, Chipolopolo anawapasha ‘mapaparazi’ wote kuwa, mapenzi yao sio ya kuchovya na kuwataka wacheze mbali na chokochoko zao zenye nia ya kuwatenganisha.


Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kibao hicho kitarekodiwa mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutambulishwa kwenye kumbi nyingi zaidi na mashabiki kukitolea maoni mbalimbali.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac