NAPOLI YACHANGANYIKIWA TETESI ZA ALLAN MARQUEZ KUTAKA KUNYAKULIWA

KLABU ya Napoli imechanganyikiwa baada ya kuambiwa kwamba kuna mchezaji wake hatari anaweza kuondoka wakati wowote.

Mchezaji huyo ni yule raia wa Brazil ambaye amekuwa na kiwango kikubwa, Allan Marquez na watu wanaomtaka kwa gharama yoyote ni klabu ya Newcastle United ya Uingereza.

Gazeti la the Sun limeandika kwamba Napoli wanaweza kumpoteza nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, kutokana na mahitaji ya Newcastle United ya sasa.

Lakini sio Newcastle peke yake, inadaiwa kuwa nyota huyo amekuwa akiwindwa kwa karibu sana na timu za Southampton na West Brom ambapo thamani yake inatajwa kuwa pauni mil 10.

Hata hivyo, Napoli wanadaiwa kuanza kuweka nguvu wakisema kuwa wanaweza kumwacha nyota huyo kama watapokea ofa ya maana kutoka timu inayomtaka.


Mkwara huo hata hivyo hauonekani kumtisha kocha Rafa Benitez ambaye anaamini kwamba akifanikiwa kupata huduma ya nyota huyo atamsaidia sana.

No comments