NEMANJA MATIC AAMUA KUJIUNGA NA JUVENTUS, ATAKA CHELSEA WAPUNGUZE BEI


Nemanja Matic sasa anataka kwenda Juventus lakini amedhamiria kuwaomba Chelsea wapunguze bei ili kurahisha uhamisho wake wa kwenda Italia.

Kiungo huyo wa Serbia anataka kuondoka Stamford Bridge kiangazi hiki huku Manchester United na Inter Milan zikimtaka lakini gazeti la Corriere dello Sport la Italia linasema nyota huyo amechagua Juventus.

Gazeti hilo limeandika katika ukurusa wake wa mbele kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 'amemwambia ndio' kocha wa Juventus Massimiliano Allegri na sasa anataka Chelsea ipunguze bei yao ya pauni milioni 40.No comments