Habari

NEMANJA MATIC KUTUA RASMI MANCHESTER UNITED WIKI HII

on

Manchester United inatarajiwa kukamilisha usajili wa pauni milioni 40 wa kiungo mkabaji, Nemanja Matic kutoka Chelsea mapema wiki hii.

Matic  ameonekana akiwa ametinga jezi ya mazoezi namba 31 ya Manchester United katika picha iliyovujishwa huku ikiaminika  kuwa ilichukuliwa wakati akijiandaa kufanya vipimo vya afya  kwenye uwanja wa mazoezi wa United – Carrington. 

Ingawa kocha wa Chelsea Antonio Conte alipendelea zaidi kumuuza Matic nje ya England, lakini duru za michezo zinabainisha kuwa vilabu hivyo vya Premier Legue vimefikia pazuri kwenye mazungumzo ya usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho  licha ya kukataa kuthibitisha juu ya ukweli au uongo wa picha iliyovujishwa, lakini aliweka wazi kuwa Nemanja Matic anataka sana kujiunga na United.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *