NEYMAR ACHEKELEA MESSI KUONGEZA KANDARASI BARCELONA

STRAIKA wa Barcelona, Neymar amesema kwamba anaona furaha kubwa nyota mwenzake, Lionel Messi kuongeza mkataba kwa kile anachodai yangekuwa majanga makubwa kama timu hiyo ingemkosa staa huyo.

Kauli ya staa huyo imekuja wakati Messi keshokutwa akijiandaa kusaini mkataba na vinara hao wa La Liga ambao utamfanya aitumikia hadi mwaka 2021.

Kutokana na hali hiyo Neymar anasema kwamba kitendo cha staa huyo kukubali kumwaga wino katika mkataba huo itashuhudiwa akimaliza kibarua chake kwenye klabu hiyo.

“Nimefurahi kuona tunaendelea kuwa na mchezaji bora duniani,” alisema staa huyo na kuongeza: “Lilikuwa ni jambo gumu kwangu kucheza soka bila yeye.”


Wakiwa chini ya kocha wao mpya Ernesto Valverde, Barca wanajiandaa kuanzisha vita mpya na mahasimu wao Real Madrid katika kuwania ubingwa msimu ujao.

No comments