Habari

NEYMAR AKINUKISHA BARCELONA BAADA YA KUPIGANA MAZOEZINI

on

Neymar amechafua hali ya hewa Barcelona baada ya kuzichapa mazoezini na mchezaji mwenzake huku usajili wake wa kujiunga na Paris Saint-Germain ukizidi kunukia.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil alizichapa na mchezaji mpya aliyesajiliwa kiangazi hiki Nelson Semedo.
Neymar amekuwa akihusishwa na uhamisho wa pauni milioni 195 kwenda Paris Saint-Germain.
Nelson Semedo beki mpya wa Barcelona alimkwatua Neymar wakati wakigombea mpira, hatua iliyofachua hali ya hewa baada ya Neymar kuchukia na kumvaa Semedo kabla Javier Mascherano hajawahi kuamua zogo.

Neymar alichukia na kususia mazoezi huku kocha Ernesto Valverde akiwa hana cha kusaidia.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *