NI KIVUMBI NA JASHO ARSENAL DHIDI YA MONACO KWA THOMAS LEMAR


ARSENAL wanamtaka Thomas Lemar wa Monaco katika usajili wa kiangazi hiki, lakini wameambiwa na klabu hiyo ya Ufaransa kuwa “hakuna makubaliano yatakayofikiwa” juu ya kuuziwa winga huyo.

Ripoti za wiki hii zimedai kuwa Arsenal ilikuwa imekaribia kukamilisha dili la kumnasa Mfaransa huyo mwenye nia ya kutua Emirates baada ya kufanya mazungumzo na Monaco wiki hii.

Kwa mujibu wa gazeti la Guardian, The Gunners iliweka mezani ofa ya karibu pauni milioni 31 kwa ajili ya nyota huyo, lakini Monaco iliwatolea nje na kumwambia Arsene Wenger kwamba mchezaji huyo hayuko sokoni.

Mabingwa hao wa Ligue 1, tayari wamempiga bei Bernardo Silva kiangazi hiki na wanakaribia kumpoteza Timeoue Bakayoko kwa Chelsea na Fabinho kwa Manchester United.

Pia kuna matamanio makubwa ya klabu kubwa za Ulaya kwa mshambuliaji wake kinda Kylian Mbappe, ikiwamo Arsenal, lakini Monaco imeamua kumpa ofa ya kuongeza mshahara wake kwa asilimia 900, ikiwa na dhamira ya kumbakisha.

No comments