NIYONZIMA KUTUA SIMBA SC NA PACHA WAKE KUTOKA TIMU YA TAIFA RWANDA

HARUNA Fadhili Niyonzima ameachana na Yanga na mahesabu yake yamekuwa yakiwasumbua baadhi ya mashabiki wake wakiwemo wale wa Yanga.

Tangu katibu mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa atangaze kwamba klabu hiyo imeachana rasmi na Haruna baadhi ya mashabiki wa Yanga wakapagawa na kuamua kuchoma jezi ya mwanasoka huyo fundi.

Simba inayohusishwa na kumsajili mchezaji huyo ikawa kimya na kuwa kama haitaki kuzungumzia jambo lake kabisa.

Lakini udukuzi wa Saluti5 umegundua kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Rwanda amemalizana kila kitu klabu ya Simba.

Mmoja wa marafiki wa mwanasoka huyo amesema kwamba Haruna hawezi kurejea Yanga kama ambavyo baadhi ya mashabiki wanasema na kama hili likifanyika maana yake atarejea kwa pesa kubwa sana.

“Kama wanadhani Haruna anarudi Yanga watakuwa wanajisumbua maana yeye amekuwa na msimamo wake na anataka kuchezea Simba,” kimesema chanzo hicho.

Rafiki huyo wa Haruna amesema kwamba mwanasoka huyo ambaye kwa sasa yupo nyumbani kwao Kigali kwa mapumziko, amemuhakikishia kwamba anakuja Simba.

“Kila kitu kiko sawa, nadhani anachongoja ni kumalizika kwa muda wake tu. Hapa kulikuwa na habari kwamba mama yake amemzuia kuondoka Yanga, sio kweli kwani mama yake anajua kuwa soka ndiyo maisha ya mwanae na Yanga mara kadhaa wameonekana kumchoka unakumbuka waliwahi kumfukuza?” amehoji.

Kwa mujibu wa rafiki huyo wa karibu, Niyonzima anakwenda Simba akiwa na pacha wake wa  uwanjani katika timu ya taifa ya Rwanda, Jean Claude Iranzi.


Habari zinasema kwamba uongozi wa Simba umeshafanya mazunfumzo na Iranzi na kutua pamoja na Haruna mwishoni na Mwezi huu.

No comments