NTAMBA BAND KUTAMBULISHWA RASMI BATOTOZ NA KIVULE WIKIENDI HII

NTAMBA Band inatarajiwa kujianikwa rasmi mbele ya mashabiki wao wa Temeke katika shoo kubwa ya utambulisho itakayopigwa Ijumaa hii ndani ya Batotoz Night Club, jijini Dar es Salaam.

Bosi wa kampuni iliyoko juu katika masuala ya burudani Bongo, Nyegera Waitu Entertainment, Dk. Ntamba na Mungu amesema wameamua kuandaa shoo hiyo ili kuiweka bayana bendi yao.

“Tumewaalika wakali wa viunno wa Khanga Moja ambao watashirikiana na wasanii wetu wa bongofleva na singeli kupamba uzinduzi huo ambao kiingilio chake kitakuwa ni sh. 4,000 tu,” amesema Dk. Ntamba na Mungu.


 Tabibu huyo amesema kuwa kesho yake, yaani Jumamosi watahamia Hanam Resort Night Club, Kivule, watakapoitambulisha Ntamba Band kwa mashabiki wao wa Wilaya Ilala.

No comments