OKWI AMPIGIA CHAPUO MGANDA MWENZAKE SIMBA SC

UKISIKIA mtu anaipenda timu mpaka halali usingizi ndio kama hivi.

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye amesaini tena mkataba wa kuichezea Simba, ameshauri klabu yake kufanya fasta kunasa saini ya kiungo mshambuliaji, Anthony Mawejje ambaye ni Mganda mwenzake.

Habari za uhakika zinasema kwamba taarifa za kusajiliwa kwa Maweje Simba ni kweli na kwamba mtu ambaye anachonga dili hilo ni Okwi mwenyewe.

Anthony Mawejje Jr alizaliwa Desemba 15, 1990, amemaliza mkataba wake wa miaka miwili katika klabu ya Knattspynufelagio prottur ya nchini Norway.


Mwanasoka huyo wa timu ya taifa ya Uganda, amezichezea pia timu za KCCA, Police Jinja na URA, zote za Uganda, lakini pia nje ya Uganda amechezea timu za IBV Vestmanjar, Golden Arrows Haugesund na Valur.

No comments