OMMY DIMPOZ ATETEA WIMBO WAKE WA "CHECHE"... asema hajauiba kokote!

STAA anayebamba kwenye medani ya bongofleva, Ommy Dimpoz amesema wimbo wake mpya wa “Cheche” hajauiba kutoka kwa msanii yeyote kama inavyoelezwa kwenye mitandao ya kijamii.

Dimpoz amesema kwamba kuanzia utunzi wa mashairi hadi mpangilio wa mashairi vyote ni mali yake na hakuna msanii mwingine yeyote mwenye mamlaka na ngoma hiyo.

“Sijui haya maneno wakati mwingine yanatokea wapi jamani, huu wimbo ni mali yangu hakuna mtu mwenye hakimiliki zaidi yangu,” alisema Dimpoz.

“Wapo watu kazi yao ni kuibua maneno kwenye mitandao ya kijamii na hasa wanapoona wimbo unafanikiwa, lakini ukweli ni kuwa hii ni kazi ya mikono yangu,” aliongeza.


Kumekuwa na uvumi kwamba wimbo huo ni mali ya Modala, hivyo Dimpoz kutuhumiwa kutumia kazi ya msanii huyo.

No comments