OMOG AWABADILISHIA WACHEZAJI WA SIMBA RATIBA YA MSOSI

KATIKA kuhakikisha kwamba kambi yao inayokuwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na umoja, kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Omog amelazimika kubadilisha ratiba ya msosi wa jioni kambini Afrika Kusini.

Simba ambayo imefika kwenye Hotel ya Petra jijini Johannesburg na wapo chini ya Omog, wachezaji wamekuwa wakipata msosi kuanzia saaa moja usiku tangu walipowasili hapo wiki moja nyuma.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi ya juzi Omog aliwaweka chini wachezaji hao na wakaambia kwamba siku hiyo na inayofuatia watalazimika kula kwa pamoja saa 12:30 jioni ambapo lazima wote wakae pamoja kupata msosi huo wa usiku.

Hali hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kurudisha umoja ndani ya timu na kuongeza morali kwa baadhi ya wachezaji


Omog alisema amelazimika kuwabadilishia ratiba wachezaji kutokana na ukweli kwamba wote walitakiwa kula pamoja na kubadilishana mawazo badala ya kila mtu kula kivyake.

No comments