OMOTOLA JALADE NAE AINGIA KWENYE KASHFA YA KUFANYA UPASUAJI WA KUONGEZA "MSAMBWANDA"

MREMBO wa filamu za maigizo nchini Nigeria anayetajwa kuwa na mvuto wa kimapenzi, Omotola Jalade nae ameanza kusakamwa na vyombo vya habari kuwa amefanya upasuaji wa kuongeza maumbile yake.

Omotola amekana taarifa hizo na kudai kuwa ndivyo alivyozaliwa na wala hafahamu lolote kuhusu upasuaji huo.
“Siwezi kufanya upasuaji kwa sababu ya kuongeza maumbile yangu, hivi ndivyo nilivyo na nitabaki kuwa hivi,” alisema Omotola.

“Najua hakuna namna naweza kuthibitisha uvumi huo lakini naomba ifahamike kuwa sijafanya upasuaji huo,” aliongeza.


Taarifa zinafichua kuwa staa huyo aliwahi kufanya ziara nchini India ambako ndiko alikokamilisha upasuaji huo.

No comments