OMOTOLA JALADE WA NOLLYWOOD ASEMA HANA MPANGO WA MARAFIKI WAPYA

STAA wa filamu nchini Nigeria ambae anatikisa soko, Omotola Jalade amesema kuwa hana mpango wa kuongeza idadi ya marafiki kwa sababu walio wengi huwa wanamchosha akili tu.

Omotola amedai kuwa kundi la marafiki alilonalo hivi sasa linamtosha kwa sababu ameshibana nao tangu enzi ya utotoni.

“Ndio. Kama kuna kitu nachukia kwenye maisha yangu ni kuwa na kundi kubwa la marafiki, sio kama sipendi watu ila sihitaji kuzunguukwa na watu wengi,” alisema Omotola.


“Marafiki nilionao sasa wananitosha kwa sababvu hawa nafahamiana nao tangu tukiwa watoto, sasa sioni haja ya kuongeza wengine.”

No comments