OMOTOLA JALADE WA NOLLYWOOD AWACHIMBA MKWARA WANAODAI AMEFANYA UPASUAJI KUONGEZA "CHURA"

KUFUATIA matukio ya kushambuliwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na suala la kuongeza maumbile yake, staa wa filamu za Nollywood, Omotola Jalade amesema yuko tayari kufungua kesi ikiwa shutuma hizo zitaendelea.

Omotola anahisiwa kufanya upasuaji na kuongeza sehemu za maumbile yake ili kutengeneza shepu yenye mvuto wa kimapenzi.

“Nilishazungumza wazi kuwa sina mpango wa kuongeza maumbile ya mwili wangu lakini hizi taarifa zinazidi kuenezwa, kama kuna mtu mwenye uthibitisho alijitokeze,” alisema staa huyo.

“Naweza kufungua kesi ikiwa suala hili litaendelea kunichafua kwenye jamii iliyonizunguuka,” aliongeza.


Omotola anatajwa kuwa staa wa kike mwenye mvuto zaidi wa kimapenzi pamoja na kuwa na jukumu zito la malezi ya watoto wake.

No comments