OZIL AKANA KUTAKA KUONDOKA EMERATES KUMKIMBIA WENGER

MESUT Ozil amekuwa akihusishwa na taarifa za kutaka kuihama Arsenal kama hatua za kupinga kuendelea kuwepo kwa bosi wake, Arsene Wenger na tetesi zilisema kuwa uamuzi huo angeufanya wakati kipindi cha usajili wa majira ya joto.

Lakini taarifa mpya zinasema kuwa Ozil amekanusha uvumi huo akisisitiza kuwa hana mpango wa kuikacha klabu hiyo na kwamba ana imani na kocha Arsene Wenger.

Kisha akasisitiza kuwa pamoja na kukanusha kutohama, pia ameweka bayana mpango wake wa kukipiga katika kikosi cha washika mitutu hao kwa kipindi kirefu.


Kwa mujibu wa taarifa za magazeti ya nchini Hispania, kwa siku mbili mfululizo yamekuwa yakiandika namna ambavyo Ozil mwenye umri wa miaka 27 alithibitisha kuwa anataka kuondoka na sababu kubwa ni kutokuwa na imani na kocha Wenger.

No comments