PATA PICHA 10 ZA UHONDO WA MASHAUZI CLASSIC ALHAMISI ILIYOPITA MANGO GARDEN


Kama kuna uhondo bab kubwa katikati ya wiki jijni Dar es Salaam, basi Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi, inahusika kwa sana kwa kila siku za Alhamisi.

Alhamisi iliyopita kundi hilo lilimimina uhondo ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni iliyoshuhudiwa na mashabiki kibao.

Kundi hilo hupatikana Mango Garden kila Alhamsi, ambapo mamia ya wakazi wa jiji la Dar humiminika hapo kupata ile kitu roho inataka.

Pata picha 10 za onyesho la Mashauzi Classic Alhamisi iliyopita.
Abdumalick akitesa na wimbo wake "Kupendwa Bahati Yangu"
 Mashabiki wakicheza wimbo "Kupendwa Bahati Yangu"
 Isha Mashauzi akitupia masauti yake matamu

Mashabiki wa Mashauzi Classic wakiwa ulingoni
 Kali Kitimoto akipapasa kinanda
 Ilikuwa pambe kama hivi
Hapa Isha akiimba rumba lake "Nimlaumu Nani"
 Mkude kwenye solo gitaa
 Saida Mashauzi akitesa na "Pendo la Ukakasi"
Shebby wa Kumwaga kwenye bass gitaa

No comments