PATCHO MWAMBA ASEMA MUZIKI WA TANZANIA UPO HATARINI


Rais mpya wa bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma”, Patcho Mwamba amesema muziki wa Tanzania upo hatarini.

Mwimbaji huyo aliyasema hayo wiki iliyopita wakati akiongea na kipindi cha Afro TZ cha Radio One kinachoongozwa na mtangazaji Rajab Zomboko.

Patcho akasema utitiri wa waimbaji wa kizazi kipya wanaotumia mfumo wa ‘play back’ wa kuimba kwa kwa kutumia CD au flash, ni hatari kwa hatma ya muziki Tanzania.

Akifafanua hilo, Patcho akasema msanii mzuri ni yule anayejua kutumia vyombo na kupiga muziki wake ‘live’.

Patcho akasema hali hiyo inatokana na upungufu au kutokuwepo kabisa kwa shule na vyuo rasmi vya muziki hapa nchini na kufanya wanamuziki wengi wategemee vipaji vya kuzaliwa.

“Kwetu Congo kuna shule na vyuo vingi vya muziki vilivyoko chini ya serikali na vinatoa vyeti vinavyofahamika kitaifa,” aliongeza Patcho.

No comments