PEDRO ASISITIZA AZMA YAKE YA KUENDELEA KUBAKI STANFORD BRIDGE

STRAIKA wa matajiri wa Stanford Bridge, Pedro amesisitiza azma yake ya kuendelea kubaki Chelsea licha ya kuwepo na taarifa kuwa anajipanga kwa ajili ya kurejea Hispania.

Pedro alijiunga na “The Blues” akitokea Barcelona kwa dau la pauni mil 21.4 lakini taarifa za sasa zinasema hana mpango wa kuondoka katika Ligi ya premier.

Klabu ya atletico Madrid imekuwa ikitajwa katika orodha ya timu zinazomwania straika huyo mwenye umri wa miaka 28.

Tetesi hizo zinatokana na hatua ya kocha Jose Mourinho kutemwa na matajiri hao ambapo bosi huyo Mreno ndie aliyemleta Pedro darajani.

Ingawa mkataba wa Pedro wa miaka minne umebakiza miezi minne tu lakini anaamini kuwa ana nafasi kubwa ya kuongeza mkataba chini ya kocha wa mpito wa Chelsea, Antonio Conte.

Akinukuliwa, Pedro amesema: “Nina miezi minne kabla ya kumaliza mkataba wangu, lakini hilo halinipi presha kwa sababu nina imani nitasalia hapa.”

“Nina furaha nikiwa hapa. Nayazungumza haya kwa imani ya moyoni. Ninajivunia kuwa katika klabu kubwa.”

“Nina furaha na mashabiki wa timu hii. Ingawa ukweli ni kwamba hali ya mambo hapa si shwari hata kidogo, lakini kwa pamoja tunaweza tukaipandisha timu kutoka hapa.”

“Ninaamini kwa kocha Antonio Conte. Ni kati ya makocha wazuri na klabu ina matarajio makubwa kwake. Najisikia vizuri.”

“Tayari ameonyesha imani kubwa kwangu, nami nina imani kubwa kwake. Ninaamini chini ya Conte timu inaweza kufanya vizuri katika kipindi kifupi,” alisisitiza Pedro.

No comments