PEDRO OBIANG AJITIA KITANZI CHA MIAKA MITANO WESTHAM UNITED

SIO jambo la ajabu sana kwa mchezaji kusaini upya katika klabu yake anayoichezea kwa maana ya kuongeza mkataba.

Ajabu inakuja pale ambapo mchezaji huyo anasaini klabu mpya huku akiwa ndie mchezaji wa kutumainiwa na klabu anayoihama.

Kiungo wa kati wa Westham United, Pedro Obiang ametia saini mkataba mwingine wa miaka mitano katika klabu hiyo, lakini akasema kwamba asingesaini mkataba mpya ni kama angepata laana.

Obiang mwenye umri wa miaka 25 alikuwa mchezaji wa kwanza kununuliwa na meneja Slaven Bilic alipojiunga na klabu hiyo ambapo alinunuliwa kutoka Sampdoria mwaka 2015.

“Kwa miaka mitano ijayo tunaweza kutimiza mambo mengi, mambo mengi,” mchezaji huyo wa zamani wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 ya Hispania amesema.

Yeye ndie mchezaji wa pili wa klabu hiyo kutia saini mkataba wa muda mrefu katika klabu hiyo katika kipindi cha wiki moja, baada ya Angelo Ogbonna pia kutia saini mkataba wa miaka mitano.

Amesema kwamba ni kweli alikuwa anawindwa na klabu mbalimbali ikiwemo Liverpool na kuna wakati alikuwa anakaribia kuondoka lakini nafsi yake ilimsuta kuachana na klabu ambayo imempa jina.


“Unajua timu hizi ni kama wazazi, kuna wakati ukiondoka kwa mbwembwe unaweza kujikuta kule unakokwenda unaishia kuwa mtazamaji,” amesema.

No comments