PEPE ASEMA ATAONGEZA MATAJI BESIKTAS


Beki wa zamani wa Real Madrid, Pepe ambaye wiki iliyopita alijiunga na Besiktas  ya Uturiki, amesema atahakikisha anaisadia timu yake mpya kuongeza mataji.

Pepe ameitaja Besiktas  aliyosaini nayo mkataba wa miaka miwili kama moja ya klabu zenye mvuto wa aina yake barani Ulaya.


Beki huyo wa kati ambaye amehamia Istanbul kwa uhamisho huru baada ya kutumika kwa muongo mmoja Real Madrid, akicheza zaidi ya mechi 300, amesema hatawaangusha mashabiki wa Besiktas.

No comments