PHIL JAGIELKA: LUKAKU AKIUZWA TU EVERTON TUMEKWISHA!

BEKI wa Everton, Phil Jagielka amedai kuwa iwapo timu hiyo itamuuza straika wao Romelu Lukaku basi kila mmoja atakayebaki itabidi afunge mabao kwani watakuwa wamepoteza mtu muhimu wa kupachika mabao.

Lukaku anategemewa kutimka Goodison Park katika dirisha la usajili wa majira haya ya kiangazi baada ya kugoma kusaini mkataba mpya katikati ya tetesi nzito zinazomuhusisha na timu ya Chelsea.

Msimu uliopita wa Ligi Kuu England, Lukaku alitumbukiza kambani mara 25, kitu kinachomtia hofu Jagielka akisema: “Akiondoka tumekwisha, lakini jukumu la kumbakisha au kutafuta mbadala wake lipo juu ya klabu.”


“Tunachosikitika, ni nani atakayeweza kufanya aliyoyafanya? Hakuna hata aliyeweza kufikisha nusu ya mabao yake na EPL inabidi iwe na watu watatu au wanne wenye uwezo wa kufunga mabao nane kwenda juu,” inabidi tusake mrithi wake haraka,” aliongeza.

No comments