PICHA 12: TWANGA PEPETA ILIVYOWEKA HESHIMA ARUSHA JUMAMOSI USIKU


Onyesho la Twanga Pepeta ndani ya jiji la Arusha Ijumaa usiku pande za ukumbi wa Triple A, limeweka heshima kubwa kwa ‘watoto’ hao wa Asha Baraka.

Ikiwa haijagusa jiji hilo kwa zaidi ya miaka saba na kufanya Arusha iamini kuwa Twanga imekufa kibiashara, bendi hiyo ikawaduwaza mashabiki wa muziki wa dansi waliofika Triple A kwa mseto mtamu wa nyimbo zao mpya na za zamani.

Wakisindikizwa na bendi mwenyeji – Rickernest Music Band (Mount Meru), Twanga wakatesa na nyimbo kama “Mtu Pesa”, “Aminata”, “Uso Chini”, “Walimwengu” na nyingine huku safu nzima ya unenguaji ikiwa  moto chini.

Hamasa iliyokuwepo kwa mashabiki ikadhihirisha kuwa muziki wa dansi bao unapendwa ila kinachohitajika ni kuboresha mbinu za kuinadi dansi ili kuendana na kasi ya soko la sasa.
 Luizer Mbutu katikati ya mashabiki
 Watu wakisebeneka na goma la Twanga
 Madansa wa Twanga wakifanya yao
 Kalala Jr jukwaani
 Ingizo jipywa kwenye safu ya waimbaji wa Twanga - anaitwa Star Boy 
 Kalala akipagawisha
 Jojoo Jumanne na God Kanuti wakchambua nyuzi za magitaa yao
 James Kibosho akizidhibiti drums
 Mandhari ya ukumbi wa Triple A
 Twanga likiendelea kunguruma ukumbini
Ally Chocky, Luizer na Kalala Jr wakiongoza safu ya waimbaji
Khalid Chokoraa akitupia rap zake kali


No comments