PICHA 12 ZA DOUBLE M PLUS IKIRINDIMA EQUATOR GRILL IJUMAA USIKU …Muumin tajiri wa sauti


Double M Plus imemimina uhondo wa burudani kwenye onyesho lao bab kubwa ndani ya Equator Grill Ijumaa usiku ambapo bosi wa bendi hiyo Mwinyuma Muumin amefunika sana kwa masauti yake matamu.

Double M Plus ikadhihirisha kuwa ina utajiri wa program ya nyimbo pendwa (hit songs) kuanzia zile za Mchinga Sound, Tam Tam na Double M Sound ambako kote huko Muumin alishiriki kuzalisha kazi nyingi zilizotesa ndani na nje ya Bongo.

Nyimbo kama “Kiu ya Mapenzi”, “Tunda”,  “Mgumba”, “Kilio Cha Yatima”, “Kisiki Cha Mpingo” na nyingine nyingi zilinguruma Equator Grill na kusisimua mashabiki waliofika kwenye ukumbi huo ulioko maeneo ya Mtoni, Temeke jijini Dar es Salaam.

 Manjegeka mwimbaji mlemavu wa macho anayetesa ndani ya Double M Plus
 Mwinyuma Muumin akitupia masauti yake matamu
 Mwimbaji wa kike wa Double M Salma Kijukuu akifanya vitu vyake
 Mzee mzima Duncan Ndumbalo akichara gitaa la kati
 Wacheza show wa Double M Plus
 Andason Said akicharaza solo gitaa 
 Kassim Said kwenye tumba
 Waimbaji wa Double M Plus
Waninga kwenye drum ... hatari sana hii namba
Kushoto ni Muddy Bass akingurumisha bass gitaa
 Muumin akiimba kwa hisia kaliNo comments