Habari

PICHA 17: CLAUDE ATUA BONGO NA KUPOKELEWA KWA KISHINDO… awaletea Watanzania zawadi ya “Usijisahau”

on

MSANII wa bongomuvi, Issa Mussa
“Claude 112” amewasili nchini jana majira ya saa nane mchana akitokea Stockholm,
Sweden alikokuwa amepiga kambi ya takriban miaka minne na kuandaa muvi yake
iitwayo “Usijisahau”.
Claude ambaye katika safari
hiyo aliambatana mkewe Amina Mussa anayeishi hukohuko Sweden, pamoja na mtoto wao,
ametua nyumbani Tanzania kwa ajili ya kuitambulisha na kuisambaza filamu hiyo.
“Kila kitu katika muvi hii
nimefanyia hukohuko nchini Sweden chini ya kampuni yangu ya AIMUS na
nimeshirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu nguli wa hapa nyumbani, kama vile Suleiman
Barafu na Wastara Juma,” amesema Claude.

“Kama kawaida ya muvi zangu
nyingi, hii pia ina maadili ya kidini kidogo na ina mafundisho mengi mno juu ya
maisha ya watu wa jamii yetu nitaisambaza kwa kulingana upepo wa soko la tasnia
yetu kwa sasa.”
DEKSHIA NAMNA MAMBO YALIVYOKUWA KUPITIA PICHA:
 Hapa baadhi ya wadau, wasanii na familia ya Issa Mussa Claude wakisubiri kwa hamu kumpokea  
 Alipowasili tu mtu wa kwanza kumrukia na kumvisha shada la maua alikuwa msanii mwenzake, Wastara Juma
 Mke wa Claude, Amina Issa akikumbatiana kwa furaha na mmoja wa wadau baada ya kuonana
 Claude na mkewe wakianza safari taratibu kuelekea Lamada Hotel walikofanya mazungumzo na waandishi wa habari
 Ghafla akakutana na mkongwe mwenzie, jacob Stephen na kulakiwa kwa furaha mno
 Hapa Amina Issa akiongea na mmoja wa waandishi aliyemvaa wakati akielekea garini
 Claude akisalimiana na Chiki Mchoma ambaye pia ni msanii mwenzie nguli
 Ndani ya Lamada Hotel mambo yalianza hivi
 Wana habari wakiwa kazini
 Claude katika picha ya pamoja na wadau, wasanii pamoja na wanafamilia wake wa karibu
 Msanii wa muziki na filamu, Thabit Abdul akiwa na mmoja wa waandishi
 Mmiliki wa mtandao wa Filamu Central, Myovela Mfwaisa akiuliza swali kuhusiana na filamu mpya ya Claude ya “Usijisahau”
 Wana habari na baadhi ya wadau wakifuatilia mazungumzo kwa makini
 Kundi la sanaa za maonyesho la “Safi” chini ya msanii Pendapenda nalo lilikuwepo kutoa burudani
 Muhseen Awadh “Dk Cheni” akiwa katika picha ya “mauzo” na msanii mwenzake, Chiki
Huu sasa ulikuwa ni wasaa wa Claude kupokea mikono ya pongezi kutoka kwa watu mbalimbali

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *