Habari

PICHA 30: MAZISHI YA SHAABAN DEDE YAITIKISA DAR ES SALAAM …mamia ya watu wajitokeza

on

Mazishi ya mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki
Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati
mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam.
Mwimbaji huyo aliyetesa kwa sauti yake tamu na kwa tungo zake za
kusisimua, amezikwa katika makaburi ya Kisutu huku idadi kubwa ya wanamuziki wa
fani mbalimbali ikiwa sehemu ya umati uliofurika makaburini hapo.
Aidha, Dede pia amezikwa na vigogo wengi wa dini ya Kiislam, maofisa
wengi wa serekali na wanamichezo maarufu.
Pengine kwa miaka ya hivi karibuni, ukiondoka msiba wa marehemu
Muhudini Gurumo, hakuna tena msiba wa mwanamuziki wa dansi uliohudhuriwa na
watu wengi kama huu wa Dede.
 Mwili wa Dede ukiswaliwa swala ya mwisho katika msikiti wa Makonde, Kariakoo
 Safari ya kuelekea makauburini inaanza
 Umati wa watu ukiondoka Kariakoo kuelekea makaburi ya Kisutu
 Kila mtu alitamani kubeba jeneza lililobeba mwili wa Dede 
 Mkurugenzi wa East African Meleody Ashraf Mohamed akiwa na mwanae njiani kuelekea Kisutu
Katikati ni kiongozi wa Msondo Said Mabela
Ras Inno (kushoto) akibadilishana mawazo na Mjusi Shemboza wa Sikinde
 Umati mkubwa wa watu ukielekea makaburi ya Kisutu
 Jeneza la Dede likiwa katikati ya umati wa watu
Sehemu ya umati mwingine wa watu 
 Aliyekuwa mwimbaji wa Chumvi Chumvi, Oscar (kushoto) akiwa na Pishuu wa Msondo
Baadhi ya wanamuziki wakiwa nje ya makaburi ya Kisutu wakisubiri mwili wa Dede
 Kaburi la Dede kabla mwili haujawasili
 Watu wa karibu wa Dede wakiwa ndani ya kaburi tayari kwa kupokea mwili wa Dede
 Mwili wa Dede ukiingizwa kaburini
 Mazishi yakiendelea
 Katikati ni mwimbaji wa zamani wa Msondo Papa Upanga
Katikati ni mwimbaji wa zamani wa Sikinde Bitchuka
 Mwenye kofia ni Hussein Jumbe
 Baadhi ya waumin walioshiriki mazishi ya Dede
Kulia ni Mohamed Mauji na Omar Teggo kutoka Yah TMK Taarab
 Salam kutoka BASATA
 Sehemu ya umati uliofurika makaburini
 Ama kwa hakika Dede amezikwa na watu wengi
 Baadhi wa wanamuziki wakiwa makaburini
 Wanamuziki wa dansi na kizazi kipya …Zahoro Bangwe, Inspector Haroun na Khalid Chokoraa
Hitimisho la mazishi ya Dede
Watu wakipata sadaka ya chakula Karikoo baada ya kutoka makaburini

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *