PRINCE AMIGO ATAMBA KUFUNIKA NA KIBAO CHAKE KIPYA JAHAZI MODERN TAARAB


WAKATI Jahazi Modern Taarab wako mbioni  kuandaa vibao vitatu vipya, bosi wa bendi hiyo, Aboubakar Soud ‘Prince Amigo’ amejinasibu kuja na kazi itakayokuwa funika bovu.

Amigo aliyepiga na ripota saluti5, anasema kuwa kama ilivyo kawaida yake, kibao chake kitakuwa cha mapenzi na kwamba humo atasikika akiwachana laivu wambea wanaowafuatilia kuwa washike hamsini zao.

“Staili ninayokuja nayo sasa hivi ni ambayo itamchanganya kila mtu atakayeisikiliza, kwasababu nataka kuonyesha kuwa kila uchao mimi ni wa kusonga mbele tu,” amesema Amigo anayefahamika pia kama ‘Bosi Kichefuchefu’.


Amigo amesema kuwa nyimbo nyingine mbili watakazoingia kambi kuandaa, moja itakuwa ni ya mwimbaji wao wa kike mwenye sauti tamu, ambaye ni mdogo wa nguli Jokha Kassim, Fatma Kassim. 

No comments