PSG YAKATA MZIZI WA FITNA JUU YA MARQUINHOS KUTUA MANCHESTER UNITED


PARIS SAINT-GERMAIN imethibitisha kuwa imemsainisha mkataba mpya wa miaka mitatu beki wake tegemeo, Marquinhos na kuzima matumaini ya Manchester United iliyokuwa ikimuwinda.

Licha ya kupata saini ya Victor Lindelof kutoka Benfica kwa dau la karibu pauni milioni 30, bosi wa Manchester United, Jose Mourinho bado ana dhamira ya kuimarisha ngome yake, huku Chris Smalling akiripotiwa kuwekwa sokoni.

Mapema Juni, taarifa nchini Brazil zilidai kuwa United iliweka mezani dau la pauni milioni 62 kwa ajili ya Marquinhos.

Lakini sasa beki huyo wa miaka 23 amezima matumaini ya United kumpeleka old Trafford kwa kujifunga mkataba wa muda mrefu na PSG.

"Mara zote nimesema nina furaha kuichezea Paris Saint-Germain, na nyongeza ya mkataba huu ni uthibitisho zaidi wa ‘kujitoa’ kwa klabu hii,” alisema Marquinhos.

No comments