Q CHILLAH AKANA KUWA NA BIFU NA TID MNYAMA

RAPA mkongwe hapa nchini, Q Chillah amesema kuwa malumbano kati yake na msanii mwenzake TID yamekuzwa sana tofauti na hali halisi iliyotokea.

Marapa hao wameripotiwa kugombana walipokuwa kwenye klabu za usiku lakini hata hivyo Q Chillah ameonekana kupinga jambo hilo jinsi lilivyoripotiwa.

“Hamna tatizo lolote kati yetu kwasababu kwanza kama ni suala la kutoleana mapovu sisi kama wasanii ni jambo la kawaida sana kwani ni hali tu ya kerekebishana,” alisema staa huyo.


“Watu wanasema tumegombana kwa sababu ya masuala ya wanawake, jamani naomba niweke wazi hatuna tatizo la namna hiyo na kiliochotokea ni kwadababu tu ya kurekebishana tabia basi hakuna lingine hapo,” alimaliza.

No comments