RAMADHANI SINGANO MESSI AJIUNGA NA KLABU YA DIFAA HASSAN D'ELJADIDA MOROCCO

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano (Messi) amemuwahi mwenzake Simon Msuva baada ya kuondoka nchini juzi kujiunga na klabu ya Difaa Hassan D’Eljadida iliyoshiriki ligi kuu nchini Morocco.

Messi ambaye mkataba wake umemalizika hivi karibuni na klabu yake ya Azam amekwenda nchini Morocco kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo yenye timu 16.

Wakati Messi akiondoka nchini humo winga wa Yanga, Simon Msuva ambaye naye anapigiwa hesabu na klabu hiyo anatarajia kuondoka nchini alhamisi hii ili kujiunga na klabu hiyo.

Meneja wa Azam, Philp Alando alipoulizwa kuhusu safari ya winga huyo alisema kuwa klabu hiyo aina taarifa na lolote lile kwa kuwa walimalizana naye toka mkataba wake umemalizika.

“Mkataba wa Singano ulikuwa umemalizika Julai 8 mwaka huu hivyo sisi hatuna mazungumzo naye yoyote na wala hatujui kuhusu safari hiyo ya Morocco wala chochote kinachoendelea,” alisema.


Wakati huo huo, klabu hiyo imezamilia kuwasajili nyotahao wawili ili kuweza kuboresha kikosi chao ambacho kinashika nafasi ya pili kwenywe msimamo wa Ligi yao ya (Botola).

No comments