KIKOSI cha timu ya Azam FC kinazidi kusambaratika baada ya mshambuliaji wake, Ramadhani Singano “Messi” kusemekana amefuzu vipimo vya afya ili ajiunge na klabu ya Al Jadida ya nchini Monaco.

Singano ambaye alitua Azam akitokea samba, amegoma kuongeza mkataba mpya kwenye kikosi hicho huku akili yake ikiangalia mbele kucheza soka la kimataifa.

Ikiwa atafanikiwa kuondoka, Singano ataingia kwenye kundi la wachezaji wenzake akiwemo John Bocco, Aishi Manura na Shomary kapombe ambao wameikacha timu hiyo wakiwa nyota tegemeo kikosini.

Azam inaweza pia kumpoteza kiungo wake tegemeo, Himid Mao ambae nae pia mkataba wake uko mwishoni na kuna uwezekano akajiunga na klabu ya Yanga ikiwa mipango yake ya kucheza soka la kulipwa Denmark itakwama.


Utaratibu mpya wa kubana matumizi kwenye kikosi cha Azam unawaweka matatani ambapo mastaa wake wakubwa kila mmoja amekuwa akitazama namna wa kubadili upepo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac