RAMSEY NOAH ASEMA HAKUINGIA KWENYE FILAMU ILI KUPATA "WACHUMBA"

GWIJI wa filamu za mapenzi nchini Nigeria, Ramsey Noah, amesema kuwa hakuwaza kuingia kwenye tasnia hiyo kwa sababu ya kunasa warembo.

Ramsey ambaye alipata mafanikio kupitia filamu ya “My Love” amesema kwamba mashabiki siku zote hudhani kuwa tabia wanazofanya kwenye filamu ndio maisha yao halisi.

“Si kweli kuwa jinsi tunavyoigiza basi ndio maisha yetu halisi. Nimekuwa nikipangwa kuigiza maneno ya mapenzi kwa sababu nayamudu,” alisema Ramsey.


“Sikuwahi kuwaza kutumia umaarufu wangu kwenye sanaa kwa sababu ya kunasa warembo, hapana! Nafanya sanaa kama kazi yangu na kitu ninachokipenda,” aliongeza.

No comments