RASHID PEMBE ACHEKELEA KUPOKEWA VIZURI NA MASHABIKI KATIKA "JAZZ SINDIMBA"

MPULIZAJI mahiri wa Saxaphone “Domo la Bata”, Rashid Pembe “Profesa” amewashukuru mashabiki wa m uziki kwa kukipokea kwa kasi kibao chake “Jazz Sindimba” alichokiachia hivi karibuni.

Akiongea na saluti5, Pembe amesema kuwa kupokelewa vyema kwa kibao hicho kunampa faraja na kumtia moyo na ari ya kujipanga kuandaa kazi nyingine nyingi zaidi.

“Jazz Sindima nilichokirekodia katika Studio za Soft Records, Dar es Salaam ni kazi ya dakika 3.26, iliyowashirikisha pia mwanangu Omary Pembe kwenye kinanda, Pishuu (Solo), Decanto Bass na mwanadada Aziz bin Love katika sauti,” amesema Pembe.

Pembe amesema kuwa kibao hicho alichokiachia rasmi wiki iliyopita, kipo katika miondoko ya ngoma ya Sindimba aliyoamua kuichanganya kidogo na miondoko ya muziki wa kisasa ili kuleta ladha tamu zaidi.


Amesema, hivi sasa yuko kwenye mchakato wa kutengeneza vibao vingine vya kikabila ambapo lengo lake kubwa ni kutangaza ngoma za kitamaduni za Watanzania.

No comments