RAYVANNY ASEMA SASA NI WAKATI WA KUZOA TUZO ZA AFRIMMA

BAADA ya ushindi wa tuzo ya BET nchini Marekani msanii kutoka kundi la WCB Raymond maarufu kama “Rayvanny” amesema sasa ni zamu ya kutwaa tuzo ya AFRIMMA Oktoba 8, nchini humo.

Waandahaji wa tuzo hizo wametangaza orodha ya wasanii watakaochuana kwenye vipengele mbalimbali ikiwa ni pamoja na msanii huyo.

Rayvanny alisema anaamini ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kwa kuwa ana vigezo vyote.


Wasanii wengine ambao wanawania tuzo hizo ni pamoja na Diamond anayewania vipengele vitano, Darasa vipengere vitatu, Ali Kiba, Lady Jay Dee, Vanessa Mdee, Tudd Thomas, Yamoto Band, Dyana Nyange na Mose Iyobo.

No comments