REAL MADRID WAKWAMA KUMNG'OA DE GEA MANCHESTER UNITED

JITIHADA zinazofanywa na klabu ya Real Madrid kumnasa mlinda mlango wa Manchester United, David de Gea zimekwama baada ya kocha Jose Mourinho kugomea uhamisho huo.


Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa kwenye tetesi za kutua Bernabeu kwa muda mrefu sasa na mara ya mwisho alishindwa kukamilisha uhamisho wake kutokana na mapungufu kwenye nyaraka.

No comments