Habari

ROMELU LUKAKU ASEMA MOURINHO AMEMFANYA KUWA MCHEZAJI ALIYEIVA ZAIDI

on

STRAIKA wa Manchester United,
Romelu Lukaku amezidi kummwagia sifa kocha wake, Jose Mourinho baada ya kusema
kuwa tayari ameshamfanya kuwa mchezaji aliyeiva.
Sifa hizo za Lukaku, 24, kwa
Mourinho zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya kukamilisha usajili wake kutoka
Everton kwenda kujiunga na Man United kwa ada ambayo inasadikika kuwa ni pauni
mil 75.
Mwanzoni mwa wiki hii staa huyo
wa timu ya taifa ya Ubelgiji aliweza kufunga bao lake la kwanza katika mchezo
ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Salt Lake katika mchezo
wa kirafiki wa kujiandaa na msimu ujao.
Baada ya kufunga bao hilo,
Lukaku ambaye msimu uliopita aliweza kufunga mabao 25 katika michuano ya Ligi
Kuu England, alisema kuwa Mourinho ambaye ni kocha wake wa zamani wakati
akikipiga Chelsea, tayari ameshafanya aimarike zaidi.
“nafahamu kile ambacho anaweza
kukifanya ndani ya timu na ni mtu ambaye amekuwa akinisukuma,” staa huyo
aliyaambia magazeti ya Uingereza.
“vilevile nimekuwa nikijituma
mwenyewe lakini yeye ndie anayenifanya kuwa mchezaji bora. Nadhani nimejifunza
mengi kutoka kwake na ninajivunia kwamba naweza kufanya kazi nae,” aliongeza
straika huyo.

“Nafurahi kwa bao langu. Lakini
bado kuna kazi kubwa ya kufanya, sisi kama timu tunafahamu tunahitaji kuwa bora
zaidi,” aliongeza.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *